Eliodori wa Altino

Panapotunzwa masalia yake.

Eliodori wa Altino (Dalmatia, leo nchini Korasya, katikati ya karne ya 4 - karibu na Venezia, Italia, 410 hivi) alikuwa askofu wa kwanza wa Altino kuanzia mwaka 380 hivi.

Alikuwa mwanafunzi wa Valeriani wa Aquileia pamoja na Kromasi, halafu aliongozana na Jeromu kwenda Nchi Takatifu alipoishi kimonaki.

Aliporudi Italia alifanywa askofu (380 hivi), ila kidogo kabla ya kifo chake alikwenda kuishi upwekeni katika kisiwa kisicho na watu [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Julai[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91153
  2. Martyrologium Romanum, Libreria Editrice Vaticana (2001) ISBN 88-209-7210-7

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search